Tuesday, March 5, 2013

Rais aliyekuwa na vituko vingi zaidi afrika pata kumjua hapa


Rais aliyekuwa na vituko vingi zaidi katika Afrika miaka ya 1970
ni hayati mzee Jomo Kenyata wa Kenya ambae mara kwa mara aliwaacha hoi na kuwavunja mbavu watu waliokuwa wakisikiliza hotuba zake.

Katika tukio moja Mzee Kenyata aliwaonya watu wanaosema kwamba ang'atuke katika siasa kwa sababu umri wake umekuwa umekwenda mno (amezeeka).

Mzee Kenyata alisema maneno haya "Ati iko mutu nasema mimi nimezeeka ? ati nimezeeka? Hebu muulizeni mama Ngina (mkewe) kama mimi nimezeeka" baada ya maneno hayo yaliyoshangiliwa sana na wananchi, mtu mmoja aliropoka kwa sauti kuu "Sawa mzee ongoza sisi tuko nyuma yako..."

Mzee Kenyata akadakia "Ati unaona hii mutu ya Mombasa! muko nyuma yangu nataka kunifanya nini? sema tuko bega kwa bega..."

No comments:

Post a Comment