Friday, May 29, 2015

Huyu ndo Sepp Blatter rais wa Fifa

Joseph Sepp Blatter alizaliwa tarehe 10 March 1936 nchini Uswis.
  Alijishughulisha na masuala ya soka toka akiwa mdogo lakini hakuwahi kuvuma kama mchezaji .
  Kuanzia mwaka 1976 alianza kujishughulisha na soka nchini Uswis katika chama cha soka cha nchi hiyo na mwaka 1981 akateuliwa kama katibu mkuu wa FIFA . Shirikisho la mpira wa miguu duniani.
  Alikuwa katibu mkuu wa shirikisho hilo chini ya raisi wa saba wa shirikisho hilo bwana Joao Havalange .
  Mwaka 1998 , ilikuwa June 8 Sepp Blatter alichaguliwa raisi wa shirikisho hilo baada ya Joao kustaafu.
  2002, 2007, 2011 alichaguliwa upya mara zote hizo.
  Leo tena tarehe 29 may 2015 Sepp Blatter amechaguliwa tena kuiongoza FIFA kwa muhula wa miaka minne ijayo.
  Anakubwa kwa kuyaleta mashindano ya kombe la dunia barani Africa mwaka 2010 na hata kuongezeka kwa timu 5 badala ya 3 katika kombe la dunia .
  Hivyo Blatter ni kiongozi ndani ya FIFA kwa miaka 18 kama katibu mkuu na 17 kama raisi wa FIFA . Kwa ujumla anaitumikia FIFA kwa miaka 35! Sasa na yeye akiwa na umri wa miaka 79!.
  Huyo ndio Blatter na FIFA yake.

No comments:

Post a Comment