Friday, December 2, 2016

El Classico kutoonyeshwa Live ndani ya England


November 29, 2016



Habari zilitoka ni kwamba mechi pendwa ya El Classico haitaonekana Live kwenye Tv za England. Mechi hii itachezwa Dec 3 na kutokana  sheria za kurusha matangazo live siku hiyo inafanya mechi hii isiruke Live ndani ya England.

Sheria zinasema kwamba hairuhusiwi mechi yoyote kurushwa live kati ya 2:45pm na 5:15pm kwa siku hiyo. zaidi ya nchi 100 watashuhudia mechi hii ambayo inawahusisha mastaa Ronaldo na Messi.

Sky Sport wataonyesha full mechi lakini watachelewa muda kidogo tofauti na kama inavyotokea live duniani kote. Rais wa La Liga alisem,“Mechi haitaonyeshwa Live ndani ya England kutokana na katazo lililo kwenye kurusha mechi live kwa muda huo. Tulikua na nafasi tatu kwa ajili ya mechi hii ambayo ni 1pm,4:15pm na 6:30pm. Baada ya kuongea na washauri wetu wametuambia tucheze kucheza 6pm itakua imechelewa sana kwa Asia na 1pm itakua mapema sana kwa America.”

“So tumechagua 4:15. Uchaguzi wa muda ni muhimu kwa kujali idadi kubwa ya watu watakao kuwa affected. Asia na America ni muhimu kuzingatia kutokana na idadi kubwa ya watu na angala ni muda fair kwa kila mpenda soka duniani.”

Mechi hii pia itawakutanisha makocha ambao waliwai kuwa wachezaji kwenye El Classico mechi za zamani.

No comments:

Post a Comment