Monday, September 10, 2018

*DC MURO AANZA NA KILIMO NA MIFUGO*Mkuu wa wilaya ya Arumeru *Mh.Jerry Muro* amewataka maafisa ugani wa wilayani Arumeru kushirikiana kwa karibu na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania *'Tanzania Agricultural Reseach Institute - TARI'* kuwezesha wakulima kulima kilimo chenye tija chenye kuzalisha mazao bora. *Dc Muro* ametoa rai hiyo, alipokutana na Mafisa Ugani wa *kata 53, kata zinazojumuisha halmashauri mbili za Arusha na Meru wilayani Arumeru,* wakati wa kikao kazi, ambacho *Mh.Muro* amekiita kikao cha mkakati wa kilimo wilayani hapa. *Mh.Muro* ameongeza kuwa, licha ya kuwa TARI inahudumia Tanzania nzima lakini kwa kuwa *Makao makuu yapo wilayani Arumeru,* kuna ulazima wa wilaya ya Arumeru, kuwa eneo la mfano, ambalo wakulima wataachana na kilimo cha *mazoea na kujikita kwenye kilimo cha kimkakati, kitakachomtoa mkulima kwenye lindi la umasikini kwa kumuwezesha mkulima wa Arumeru kulima kilimo* chenye kutumia mbegu bora na kuweza kupata mazao bora. Aidha *Dc Muro* amesema kuwa lengo lake, katika kuelekea uchumi wa viwanda ni kuhakikisha *wakulima wa Arumeru, wanalima kilimo cha kimkakati chenye kutumia mbegu bora na kupata mazao bora yenye uwezo wa kuchakatwa na kuongezewa thamani kupitia viwanda vyetu vya ndani* na kuuzwa kama bidhaa ghafi na si kuuza mazao kama ilivyozoeleka. Na kuagiza Maafisa hao kuandaa taarifa itakayoonesha idadi ya *wakulima waliopata ujuzi ikiwa na namba zao za simu ili aweze kuwasiliana nao* kuthibitisha endapo ni kweli wakulima hao kupata ujuzi huo wa kilimo. Naye Meneja wa *kituo cha utafiti wa *kilimo Tanzania -TARI* amesema kuwa, yuko tayari kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na *Mkuu wa wilaya ya Arumeru,* kwa lengo la kuhakikisha wakulima wanalima kimkakati na kuwezesha nchi yetu kuelekea *uchumi wa viwanda huku kilimo* hicho kikimnufaisha mkulima kwa kumuongezea kipato. Pia amefafanua kuwa, Taasisi hiyo inatoa huduma kwa watanzania wote ikiwemo *wakulima binafsi, taasisi binafsi na za serikali pamoja na makampuni hivyo ni dhahiri kupita watalamu wa taasisi hiyo,* wakulima wananafasi kubwa ya kubadili aina ya kilimo na kulima kilimo chenye tija. Ametaja mazao yanayofanyiwa tafiti ni pamoja na *mazao ya mboga, matunda na mazao ya mizizi na kuongeza kuwa, kupita tafiti hizo wamefanikiwa kupata mbegu bora na zinazozalishwa mazao bora.* Hata hivyo *Maafisa Ugani hao, wamempongeza mkuu huyo wa Wilaya,* kwa kukaa nao kirafiki na kuwatia moyo juu ya utekelezaji wa majukumj yao,na zaidi kupanga mikakati na mipango ya pamoja, yenye lengo la kuboresha *hali ya kilimo kwa manufaa ya wananchi wa Arumeru* na taifa kwa ujumla. *Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru* *#WakatiWetu* *#MeruYetu* *#TanzaniaYetu*

No comments:

Post a Comment